Ni Club mpya ya michezo inayojumuisha WANAFUNZI WAVYUO VYOTE na WANANCHI wapenda michezo katika  jijini DODOMA.

Club hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumapili ya tarehe 28/01/2024 katika Uwanja wa Mpira wa Shule ya Msingi Makole kuanzia Saa 12:00 Alfajiri hadi Saa 3:00 Asubuhi.

Katika siku hiyo ya uzinduzi wa club hii mpya katika jiji la Dodoma  kutakuwa na shughuli mbali mbali zitakazofanyika uzinduzi huo, shughuli hizo zitakuwa ni pamoja na:

  1. Mazoezi ya Viungo “Aerobics”
  2. Jogging Km 10. (Makole S/M, CBE, Uzunguni, Round About “Safina House”, Round About “Kimbinyiko”, Saba Saba, Makole S/M).
  3. Maelezo mafupi ya kuijua club ya SEPESHA RUSHWA SPORTS & JOGGING CLUB na malengo ya kuanzishwa kwake.
  4. Usajili wa wanachama wapya wa SEPESHA RUSHWA SPORTS & JOGGING CLUB, katika usajili huu utakaofanyika siku hii ya uzinduzi kutakuwa na usajili kwa bei maalum ya ofa kwa wale watakaokuwa tayari kujiunga na club hii ya SEPESHA RUSHWA SPORTS & JOGGING CLUB.

Gharama ya Usajili (OFA MAALUM)

  1. Wanachuo (Wanafunzi) – Tshs 10,000/=
  2. Watu wazima                   – Tshs 15,000/=

Kwa watakaosajiliwa siku hii ya uzinduzi wa SEPESHA RUSHWA SPORTS & JOGGING CLUB na kulipa bei hiyo ya ofa, watapata  Fomu ya Kujiunga na club, watapata Tshirt ya Club na Medali.

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huu wa SEPESHA RUSHWA SPORTS & JOGGING CLUB anatarajiwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Jabir Shekimweri.

WOTE MNAKARIBISHWA

Michezo ni Afya, Umoja na Maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *