Nani anastahili kuwa Balozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa Tanzania (ACVF AMBASSADOR?

Mtu yeyote bila kujali umri, jinsia na kazi anayofanya na mahali alipo anaweza kuwa Balozi wa Sauti ya wapinga rushwa Tanzania (ACVF Ambassador) ili mradi tu ajisajili.

 

Hamasa ya kujisajili kuwa Balozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa Tanzania (ACVF AMBASSADOR)

Mnamo tarehe 11/07/2023 katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mapambano dhidi ya rushwa Afrika iliyofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa AICC na kuhudhuriwa na mataifa Zaidi ya 13 barani Afrika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN alipongeza jitihada zetu katika kuisadia Serikali yake katika mapambano dhidi ya rushwa na kutuagiza kuongeza idadi ya mabalozi wa sauti ya Wapinga Rushwa Tanzania nch nzima chini ya mwavuli wa taasisi yetu ya ANTI CORRUPTION VOICES FOUNDATION na kufungua ofisi zingine nyingi za mikoa na kanda za taasisi.

Ni kwa njia zipi ninaweza kujisajili kuwa Balozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa Tanzania (ACVF AMBASSADOR)?

i. Gharama za kujisajili kuwa Balozi ni Tshs 15,000/= (Elfu kumi na tano tu) ambapo Tshs 3,000/= ni gharama ya Kitambulisho na Tshs 12,000/= ni ada yako ya ubalozi kwa mwaka mzima. Malipo haya yanaweza kufanyika kwa awamu moja au mbili tu kwa mwaka.

ii. Baada ya kukamilisha usajili na kulipa ada, Utatambulika kama Balozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa kwa kupewa Kitambulisho rasmi.

iii. Usajili wa mabalozi na malipo unafanyika kwa njia kuu mbili:

      a. Njia ya kwanza ni kwa kupitia tovuti ya taasisi yetu ambayo ni: anticorruptionvoices.or.tz.

      b. Njia ya pili ni kupitia kwa Viongozi wenyeviti/Makatibu wa mikoa kwa sasa ni mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu, Ezekiel Godwin Lesikar simu namba – 0789 866760, mkoa              wa Dodoma Ndugu, Eliasa Abdallah Hussein simu namba – 0621 431114 na mkoa wa Arusha Ndugu Timotheo Kija Malemo simu namba – 0786 380214.

          Kupitia kwa viongozi hawa utajaza fomu sawa sawa na iliyoko kwenye tovuti na kufanya malipo ya kitambulisho chako na ada.

Ni manufaa gani napata kujisajili kuwa Balozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa Tanzania (ACVF AMBASSADOR)?


i. Utapata Elimu ya Rushwa itakayotolewa kwa Mabalozi kila wakati kwa njia mbali mbali.
ii. Elimu hii itakupa ujasiri na kuwa mzalendo kuzuia vitendo vya rushwa vinavyofanyika mbele yako kwa kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu za nchi.
iii. Utakuwa na fursa kubwa ya nafasi za kazi na za kujitolea kwa taasisi pale inapojitokeza.
iv. Utakuwa umejiunga na jumuiya(Network) kubwa ya watanzania wazalendo ambao ni mabalozi katika mapambano dhidi ya rushwa Tanzania.
v. Itakupa fursa ya kushiriki mikutano, semina na matamasha mbali mbali ya kuwajengea uwezo mabalozi wa Sauti ya wapinga rushwa Tanzania.
vi. Itakujengea kuwa na Maadili na Mzalendo halisi katika maisha yako na shughuli zako za maisha ya kila siku.
vii. Inakupa nafasi ya kuwajibika kama balozi wa sauti ya wapinga rushwa Tanzania po pote pale unapokuwepo vyuoni, mtaani, kazini kwako na kwingineko kote.
viii. Kutakuongezea wasifu wako (CV’s) yako ambapo itakusaidia kuweza kuaminika sehemu mbalimbali kwani utajengwa zaidi kuwa mzalendo na mwadilifu.
ix. Rushwa ni Adui wa Haki hivyo kushiriki katika kuizuia, kuelemisha na kuidhibiti utakuwa umeiunga mkono Serikali kwenye mapambano dhidi ya rushwa jambo ambalo ni jukumu la kila raia.
x. Utapata nafasi ya kushiriki kampeni na miradi mbalimbali itakayo anzishwa na taasisi ya Mabalozi wa Sauti ya Wapinga Rushwa Tanzania.
xi. Utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupata hudumu na motisha ambazo zinatolewa na taasisi mfano vyeti vya pongezi na shukrani kulingana na utendaji wako kama balozi na ushiriki wako katika semina na mafunzo mbali mbali yatakayofanyika.
xii. Utapata nafasi ya kushauri na kupendekeza maboresho ya utendaji wa taasisi na mabalozi kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *