TAARIFA YA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA VIWANJA VYA NYERERE SQUIRE – DODOMA TAREHE 05 – 10/12/2023


1.0 UTANGILIZI:


ACVF ni Asasi ya Kiraia (NGO) inayoundwa na vijana wazalendo wa Kitanzania walioamua kuanzisha taasisi hii kwa lengo la kuelemisha na kuhamaisha raia wa Tanzania kujizuia na vitendo vya rushwa. Vijana hawa ni vijana waliokuwa kwenye vilabu vya wapinga rushwa vyuoni baada ya kuhitimu masomo yao wakaamua kuanzisha taasisi hii kwa ili kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa.

ACVF imesajiliwa tarehe: 03 Julai, 2020 kwa nambari ya Usajili: 00NGO/R/1205. Usajili umefanywa chini ya Kifungu cha 11(1) na 17(2) cha Sheria Na. 24 ya 2002. ACVF kwa mujibu wa usajili, imesajiliwa kufanya kazi Tanzania Bara.

 

2.0 KAZI ZA MSINGI ZILIZOFANYWA NA TAASISI KUANZIA DESENBA 2022 HADI NOVEMBA 2023.

 

i. Kufanya uzinduzi wa kampeni ya BADILI TABIA #SepeshaRushwa kwa mikoa ya Dar Es Salaam, Dodoma na Arusha.
ii. Kufanya kampeni ya BADILI TABIA #SepeshaRushwa kwenye maeneo mbali mbali, kwenye mikutano, matamasha, vyuoni na kwenye mitandao ya kijamii.
iii. Kushiriki mikutano mbali mbali na kufanya maonyesho ya shughuli tunazofanya za uelemishaji.
iv. Kuandaa mbio za SEPESHA RUSHWA MARATHON kwa awamu mbili sasa 2022 na 2023 kwa mafanikio makubwa..
v. Kuendelea kuwasajili Mabalozi wa Sauti ya Wapinga RushwaTanzania (ACVF AMBASSADORS) na mpaka sasa wamefika mabalozi 1240 nchi nzima.

3.0 TAARIFA YA HUDUMA ZILIZOTOLEWA KWENYE WIKI YA MAADILI, UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU.


I. Idadi ya waliohudhuria kwenye banda ni watu 112 .KE 50 na ME 62
II. Huduma zilizotolewa kwenye banda letu.

 

Huduma tuliyotoa kwenye banda letu ilikuwa ni:
  a. Uelemishaji wa mambo ya rushwa na madhara yake katika jamii yetu,
  b. Ushauri wa mambo mbali mbali kulingana na maswali waliyoulizia wageni wetu,
  c. Maonyesho na mauzo ya bidhaa zetu tulizotumia kwenye SEPESHA RUSHWA MARATHON 2023 kama vile Track suti, Tshirts na Medali zilizotumika.


III. Malalamiko yaliyotolewa kwenye banda letu na namna tulivyoyashughulikia:
  1. Malalamiko ya Ndoa, Kunyanganywa watoto, na kutokupewa haki ya kumwona. Mhusika alishauriwa kuwaona wahusika wa wizara ya Sheria na Katiba.
  2. Malalamiko ya kupewa Likizo ya ugonjwa mwalimu, lakini baada ya muda alipata barua ya kusimamishwa kazi. Aliashauri kwenda tume ya utumishi wa umma.
  3. Malalamiko ya maeneo kuvamiwa na watu wasiowajua huku wakiwa na hati za umiliki wa maeneo hayo wakati wao wamezaliwa hapo na hatimaye walivunjiwa nyumba zao. Walishauriwa kwenda kuwaona wahusika wa wizara ya Ardhi.


IV. Malalamiko yaliyoelekezwa Mamlaka zingine:
  a. Malalamiko ya Ndoa tulielekeza Wizara ya Katiba na Sheria.
  b. Malalamiko ya Likizo ya Ugonjwa na Kusimamishwa kazi tulielekeza Tume ya Utumishi wa Umma.
  c. Malalamiko ya watu kuvamiwa maeneo yao na kuvunjiwa nyumba tulielekeza Wizara ya Ardhi.


V. Viongozi waliotembelea banda letu.
  1. Mgeni Rasmi Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Msafara wake.
  2. Sivangilwa S. Mwangesi Kamishna Mkuu Tume ya Maadili.
  3. Kasamsa Kisembe DC Njombe.

  4. Amina Tali Ali Kamishna THBUB DODOMA.

  5. Dkt. Thomas P. Masanja Kamishna THBUB DODOMA.

 

VI. Maelekezo yaliyotolewa na viongozi walipopita kwenye banda letu:
Viongozi waliotembelea banda letu wote walitoa Pongezi kwa kazi nzuri tunayoifanya ya kuisadia Serikali katika mapamabano dhidi ya rushwa na kutuhamasisha kuongeza bidii katika kazi zetu bila kukata tamaa.

4. MAJUKUMU YA TAASISI YETU YA ACVF KISHERIA.


i. Kukuza utamaduni wa uwazi, uwajibikaji na uadilifu katika ngazi zote za jamii ya Kitanzania.
ii. Kukuza uwajibikaji, Utawala Bora na uwazi.
iii. Kujenga uelewa wa kutosha wa Umma kuhusu rushwa na madhara yake.
iv. Kuimarisha jamii ili kuzuia na kupambana na aina zote za rushwa.
v. Kuhimiza Jamii kuwa tayari kuchukua hatua dhidi ya rushwa.
vi. Kutoa usimamizi wa umma na watendaji wa kisiasa ili kupambana na rushwa kikamilifu.

5. MGENI RASMI.

Mgeni rasmi katika hitimisho la wiki hii ya Maadili, Haki za Binadamu na Utawala Bora alikuwa ni Mh. Kassim Majaliwa Kassim – Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alitukabidhi pia alitukabidhiCheti Cha Utambuzi wa huduma zilizotolewa na taasisi yetu ya ACVF katika wiki hiyo.


Waziri Mkuu alitumia hadhira hii pia kufanya uzinduzi rasmi wa MKAKATI WA TAIFA DHIDI YA RUSHWA NA MPANGO WA UTEKELEZAJI AWAMU YA NNE maarufu kama NACSAP IV na sisi kupewa nakala mbili kwa ajili ya kuisoma na kuifanyia kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *